Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Arumeru na Wilaya ya Arusha  imemtaka Mbunge wa  Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema, oktoba 24 mwaka huu kupanda kizimbani kusomewa maelezo ya awali ya mashtaka mawili ya makosa ya jinai yanayomkabili yaliyotokea mwishoni mwa mwaka jana .

Kesi hizo ni namba 440/2016 na 441/2016 za uchochezi dhidi ya Rais John Pombe Magufuli.

Ambapo Oktoba 23, 2016 katika mkutano wa hadhara viwanja vya shule ya Sekondari Baraa, na oktoba 22 mwaka huu katika eneo la kambi ya Fisi kata ya Ngarenaro, Lema alitoa kauli zisizofaa dhidi ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

Kesi hizo zilifunguliwa jana kwa ajili ya Lema kusomewa maelezo ya awali na kuhairishwa baada  ya Wakili wa Lema Sheck Mfinanga kuielezea mahakama mteja wake yuko safarini  Kenya.

Baada ya utetezi huo Wakili wa Serikali, Fotunatus Mhalila, aliiomba mahakama kuhairisha kesi hiyo ili iweze kupanga tarehe nyingine mshatikiwa aweze kusomewa maelezo ya awali.

Aidha Hakimu Mkazi, Jasmin Abdul, alikubali ombi na kuahirisha kesi hiyo mpaka oktoba 24 mwaka huu.

 

Video: Real Madrid yaangukia pua, yapigwa na Real Betis
Man City, Man Utd, Arsenal na Chelsea zasonga mbele Carabao Cup