Mbunge wa Arusha mjini (Chadema), Godbless Lema, amesema Serikali  ifikirie namna ya kuwatenga madaktari na wauguzi wanaowahudumia wagonjwa wa virusi vya Corona ili kulinda familia zao na maambukizi ya ugonjwa huo.

Amesema hayo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twetter huku akitolea mfano nchi ya Kenya ambayo madaktari na wauguzi  wamepatiwa nyumba maalumu za kujitengana na familia zao ili kuepusha kusambaa kwa maambukizi.

”Kenya kuanzia sasa madaktari na wauguzi wanao wahudumia wagonjwa wa Corona virus watakuwa wanaishi nje ya nyumba zao kwa gharama ya serikali ili kulinda familia zao na maambukizi ya ugonjwa huu. Ni utaratibu wa maana uliojaa upendo. Tufikiri namna hii pia,” ameandika Lema.

Mpaka sasa wizara ya afya kwa kushirikiana na serikali imeendelea kutoa elimu kwa wananchi jinsi yakujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa Covid 19 ambapo Tanzania imeripoti visa 24.

Rage: Simba wakabidhiwe ubingwa
Benki yashikilia nyumba za Jeff Koinange kupigwa mnada