Mbunge wa Kahama, James Lembeli ameweka wazi sababu zilipelekea kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Akiongea na waandishi wa habari jana mjini Kahama, Lembeli alisema kuwa sababu kubwa ni kuhujumiwa mara kwa mara baadhi ya viongozi wa CCM na vitendo vya rushwa vinavyotawala michakato mbalimbali ya chama hicho.

“Nilikipenda lakini nimelazimika kuchukua uamuzi huu mgumu. Najua imewauma, imewakera wengi lakini naomba na wao waangalie hali ambayo viongozi wa Chama Cha Mapinduzi katika wilaya ya Kahama wamepandikiza kwangu. Sikupenda kufanya hivyo lakini imebidi nifanye uamuzi huu mgumu,” alisema.

Aliongeza kuwa katika kipindi chake cha miaka tisa ya ubunge, anamshukuru Rais Kikwete kwa kusaidia kuhakikisha jina lake linarudi na anagombea nafasi ya ubunge mwaka 2010 licha ya kuwa viongozi wa ngazi ya wilaya ya chama hicho walikuwa wameliondoa kwa fitina.

“Nashukuru Chama Cha Mapinduzi kwanza kwa kunilea na kwa kunifikisha hapa nilipo. Lakini kwa kulea wizi, kwa kulea rushwa, kwa kulea mizengwe mimi binafsi niliona kabisa sina nafasi katika jamii hiyo,” tunamnukuu Lembeli.

Katika hatua nyingine, James Lembeli alitumia fursa hiyo sio tu kutangaza kujiunga rasmi na Chadema bali kutangaza pia nia ya kugombea ubunge tena kwa tiketi ya chama chake hicho kipya.

Meek Mill Amponda Drake, Amkejeli Kwa Picha Aliyopozi Na Nicki Minaj
Kenyatta Awatoa Hofu Wakenya Kuhusu Ziara Ya Obama Na Ushoga