Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli, ameitaka Serikali iunde tume huru ya kuchunguza sakata la Faru John na kwamba yuko teyari kutoa ushirikiano anajua ukweli kuhusu suala hilo.

Aidha, amesema kuwa tume iliyoundwa kwa sasa haiwezi kuja na ukweli kuhusiana na sakata hilo la Faru John kupotea.

Ameyasema hayo alipokuwa akihutubia wananchi wa Kata ya Isagehe Halmashauri ya Wilaya ya kahama kwenye mkutao wa kampeni za kumnadi mgombea udiwani wa Chadema, Richard Luziga.

“Ndugu zangu wananchi napenda kuzungumzia sakata la Faru John, naitaka Serikali iunde tume huru itakayojumuisha viongozi wa dini kuchunguza suala hilo na mimi nipo tayari kutoa msaada wangu kwa sababu hao aliowateua Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, kuchunguza suala hilo hawatampa ukweli,”amesema Lembeli.

Hata hivyo, Lembeli amesema viongozi aliowatuma Waziri Mkuu Majaliwa, kushughulikia suala hilo hawata weza kumweleza ukweli, hivyo anaiomba Serikali iunde tume huru kwaajili ya kushghulikia suala hilo..

Helmeti yatajwa kuwa chanzo cha maradhi
Makamba kutikisa Zanzibar