Aliyewahi kuwa Mbunge wa Kahama James Lembeli, amesema kuwa atafikisha kwa Rais Magufuli majina ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), waliofanya ufisadi  wa zaidi ya sh. mlioni 130 za mfuko wa jimbo hilo.

Ameyasema hayo katika kampeni za kumnadi mgombea wa udiwani wa kata ya Isagehe, Richard Luziga, amesema kuwa ndani ya CCM kumetawaliwa na dhuluma iliyoota mizizi ambayo itamshinda kuitoa mwenyekiti wake.

“Sasa hivi naandaa orodha ya majina ya viongozi wa CCM kwa maana ya watendaji wa vijiji ambao walichukua pesa yangu na ya mfuko wa jimbo, nampelekea Rais Magufuli mwenyewe tuone kama atawatumbua na majina yao ntayaweka hadharani,”amesema Lembeli.

Aidha, amesema kuwa ndani ya CCM viongozi ni mafisadi, katika kipindi chake cha ubunge walimkwamisha kupigania maendeleo ya wananchi kwa baadhi yao kutafuna fedha hizo sambamba na mabati ambayo aliyatoa kwa nguvu zake binafsi.

Kwa upande wake mgombea udiwani wa kata ya Isagehe, Richard Luziga amesema kuwa ata hakikisha anapigania maendeleo kwa kuishinikiza serikali iwaondolee kero ya maji,Zahanati na nishati ya umeme.

 

Man Utd, Everton Zamponza Mike Dean
Tobias Kifaru: Simba Hawatoki Jamhuri