Albam ya Beyonce, Lemonade aliyoitoa bila kelele nyingi za promo imeweka historia katika muziki baada ya nyimbo zake 12 kuingia kwenye chart ya Hot 100 kwa wakati mmoja.

Beyonce amekuwa mwanamke wa kwanza kuwa na nyimbo 12 au zaidi kwenye chart hiyo tangu ianzishwe.

Kama hiyo haitoshi, albam hiyo ya Mama Blue Ivy amepata fursa ya kutunukiwa heshima ya mauzo ya ‘Platinum’ na RAA ikiwa ni muda mfupi baada ya kushinda tuzo ya mitindo ya CFDA (CFDA Fashion Icon Award).

Hivi sasa Beyonce anaendelea na ziara yake ya ‘Formation World Tour’ akipewa sapoti ya karibu na mumewe, Jay- Z.

JPM kuongoza maadhimisho ya Kimataifa ya watu wenye ualbino
Video: Yametajwa Majina Ambayo siyo sahihi kuyatumia kwa watu wenye Ualbino