Bingwa wa ndondi duniani, Lennox Lewis pamoja na Muigizaji nguli duniani, Will Smith wameteuliwa kuwa miongoni mwa watu watakaobeba jeneza lenye mwili  wa aliyekuwa bingwa wa dunia wa ngumi za uzito wa juu mara tatu, Muhammad Ali.

Wawili hao wataungana na Jerry Ellis, kaka yake marehemu, Jimmy Ellis, John Grady, Jan Wadell na Komawi Ali.

Lewis ana historia ya kushinda ubingwa wa dunia wa uzito wa juu mara tatu sawa na Muhammad Ali aliyefungua pazia la historia hiyo. Naye Will Smith amepewa nafasi kutokana na ukaribu wake na familia ya Muhammad Ali baada ya kuigiza filamu ya maisha yake mwaka 2001.

Will Smith (kulia) katika filamu aliyoigiza kama Muhammad Ali

Will Smith (kulia) katika filamu aliyoigiza kama Muhammad Ali

Muhammad Ali alifariki Juni 4 mwaka huu akiwa na umri wa miaka 74. Mazishi yatafanyika Ijumaa hii katika mji aliozaliwa wa Louisville, Kentucky.

Lewis (kushoto) na Muhammad Ali

Lewis (kushoto) na Muhammad Ali

Video: Waziri Majaliwa aziomba nchi lilizoendelea kushirikiana na Tanzania katika kuwahudumia Wakimbizi
Video: Serikali yatangaza TTCL kufanya mambo makubwa kuanzia mwezi Septemba

Comments

comments