Kituo cha msaada wa sheria na haki za binadamu LHRC kimepokea msaada wa bilion 4 za kitanzania kutoka kwa balozi wa Norway Nchini ili kuimarisha utekelezaji wa  majukumu ya kituo hiko, huku ikiwa ni njia mojawao ya kukuza mahusiano mazuri yalipo katika hizi nchi mbili.

Akizungumza jana mbele ya Mkurugezi wa LHRC na wanahabari balozi Hanne Marie Kaarstad amesema Msaada huo ni katika hali ya kutambua mchango wa kito hicho ambapo ripoti zinaonyesha mchango mkubwa hasa katika kusaidia jamii dhidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu

LHRC imeonesha uwezo mkubwa wa kusimamia haki  katika utendaji wake wa kazi na wameonesha kuwa mstari wa mbele katika jamii kuonesha jinsi gani kituo hicho kina umuhimu tangu kimeanza kupokea msaada kutoka Norway 2004 Alisema Balozi Hanne Marie.

Aidha Mkurugenzi wa LHRC  Dk. Hellen Kijo-Bisimba baada ya kupokea fungu hilo kutoka kwa Ubalozi  wa Norway ametoa shukrani zake za dhati na kusisitiza kuwa fedha hizo zitatumika hasa zitatumika katika kuangazia masuala yote yahusuyo jamii.

kijooo

”Fedha tulizopokea tutahakikisha zinatumika haswa katika kuitetea na kudai mchakato wa  katiba mpya, pamoja na kuangazia mwenendo wa bunge kwa ujumla pia kuendeleza miradi iliyopo kwenye tume ikiwa ni pamoja na kupinga na kupiga vita ukatili wa aina yoyote kwenye jamii” Alisema Kijo-Bisimba

 

Uingereza Kuondoka EU?
Victor Wanyama Amfuata Mauricio Pochettino Jijini London