Licha ya shinikizo la chama chake cha ANC kumtaka kuachia madaraka, Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amesema hana nia ya kujiuzulu na kwamba ataendelea kupambania mamlaka yake na kwamba ataipinga ripoti ya bunge mahakamani na kulinda wadhifa wake kisheria.

Kwa mujibu wa msemaji wa Rais, Vincent Mangwenya amesema Ramaphosa anakabiliwa na shutuma baada ya mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi kuwasilisha malalamiko Polisi akidai rais huyo hakuripoti wizi uliotokea mwezi Februari mwaka 2020 katika shamba lake kaskazini mashariki mwa nchi.

Moja ya picha zilizopo katika shamba binafsi la Phala phala lilotajwa katika tukio la mabilioni ya pesa.

Katika malalamiko hayo, Ramaphosa pia anadaiwa kuwa alipanga juu ya kutekwa nyara wezi hao na kisha kuwahonga ili kuwaanyamazisha, jambo ambalo Rais Ramaphosa amekana kuhusika nalo licha ya uwepo wa kashfa dhidi yake na taarifa za kupatikana zaidi ya dola nusu milioni zilizofichwa kwenye mito ya makochi.

Hata hivyo, tarifa hizi zinakuja wakati mbaya ambapo Desemba 16, 2022 Ramaphosa anatarajia kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama tawala cha African National Congress (ANC), nafasi muhimu itakayomuwezesha kusalia kama rais wa taifa la Afrika Kusini endapo atashinda.

Urusi 'yatunisha msuli' ukomo bei ya mafuta
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Decemba 4, 2022