Ligi Daraja la Pili Tanzania Bara (SDL), inatarajiwa kuanza Septemba 30, mwaka huu kwa timu kuchuana katika viwanja vitano tofauti.

Kwa mujibu wa Ratiba,  michezo ya siku hiyo itakuwa ni kati ya Abajalo na Cosmopolitan; Namungo na Reha kutoka Kundi A wakati kundi B kutakuwa na mchezo kati ya Pepsi na Madini.

Kundi C kutakuwa na mchezo kati ya Burkinafaso na Ihefu kadhalika Boma itacheza na Mkamba Rangers huku Kundi D likikutanisha timu za Bulyanhulu na Milambo.

Katika Kundi hilo la D Mchezo kati ya Nyanza FC na Area C uliokuwa ufanyike Septemba 30, 2017 siku ya Jumamosi kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, sasa utachezwa Oktoba 01, 2017 siku ya Jumapili kwenye Uwanja huo huo.

Sababu za mabadiliko haya ni kutokana na mchezo kati ya Pepsi FC vs Madini FC kuchezwa tarehe 30.09.2017 katika uwanja huo. Awali mchezo wa Nyanza na Area C ulipangwa kufanyika mkoani Manyara, lakini kutokana na hali ya uwanja ilibidi Bodi ya ligi ufanye mabadiliko husika.

Watu 44 wakamatwa na jeshi la polisi Tabora
Naibu waziri Anastazia Wambura aitaka TFF kushirikiana na serikali kuleta maendeleo ya soka