Ligi Daraja la Pili (SDL) nchini inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa timu zote 24 kucheza katika viwanja mbalimbali, kusaka timu nne za juu kutoka kila kundi zitazokpanda ligi daraja la kwanza msimu ujao.

Jumapili Kundi A, Mvuvumwa FC watawakaribisha Singida United katika uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma,  Mirambo FC watacheza dhidi ya Green Warriors uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, huku siku ya jumatatu Abajalo Tabora wakichuana dhidi ya Transit Camp katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Kundi B, Jumapili Pamba FC watacheza dhidi ya Alliance Schools uwanja wa CCM Kirumba, JKT Rwamkoma watawakaribisha AFC ya Arusha kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma, huku siku ya Jumatatu  Bulyanhulu FC wakicheza dhidi ya Madini FC kwenye uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.

Kundi C, Jumatatu Mshikamano watawakaribisha Cosmopolitan uwanja wa Karume jijini Dar es salaam, Karikaoo FC watawakaribisha Villa Squad uwanja wa Ilulu mjini Lindi, huku Changanyikeni wakicheza dhidi ya Abajalo Dar kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.

Kundi D, Kesho Jumamosi African Wanderes watawakaribisha The Mighty Elephant uwanja wa Wambi Mafinga, Jumapili Mkamba Rangers watacheza dhidi ya Sabasaba, huku Wenda FC wakicheza dhidi ya Mbeya Warriors katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Mgombea urais Uganda aahidi kumrudisha Idi Amin Uganda, Waislam wapinga
TFF Yatuma Salamu Za Rambirambi Kwa Dambaya