Ligi kuu ya soka Tanzania Bara inaendelea tena leo kwa mchezo mmoja, ambapo Stand United (Chama La Wana) watakuwa kwenye dimba lao la nyumbani la CCM Kambarage mkoani Shinyanga kuwaalika Ndanda FC kutoka mkoani Mtwara.

Timu hizo zinaingia kwenye mchezo wa leo zikiwa zimetofautiana kwa alama mbili pekee katika msimamo wa ligi kuu.

Stand United wanashika nafasi ya 8 wakiwa na alama 32 huku wapinzani wao Ndanda FC wakiwa katika nafasi ya 13 baada ya kujikusanyia alama 30, huku timu zote zikiwa zimeshacheza michezo 27.

Stand United wanaingia katika mchezo wa leo wakiwa na kumbukumbu ya kutoka sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar katika mchezo uliopita, huku Ndanda FC wao wataingia kwenye dimba la CCM Kambarage wakiwa na kumbukumbu ya kuchapwa mabao 4-2 na Mwadui FC katika mchezo uliopita huko Mwadui Complex.

Gianluigi Buffon: Tunaitaka Real Madrid Nusu Fainali
Abdi Banda Yupo Huru