Sherehe zimepita, Maandalizi yamefanyika baina ya timu zote zinazoshiriki Ligi kuu ya NBC na Jana Jumatatu (Agosti 15) ilianza rasmi kwa michezo miwili kuchezwa katika viwanja na majira tofauti.

Ihefu FC waliikaribisha Ruvu Shooting katika Uwanja wa Highland Estate Mjini Mbarali mkoani Mbeya majira ya saa 10:00 jioni huku Namungo nao waliwaalika Mtibwa Sugar kutoka mkoani Morogoro Majira ya saa 1:00 usiku Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Ihefu FC iliyorejea Ligi Kuu ikitokea Ligi Daraja la Kwanza, ilianza vibaya michuano hiyo baada ya kukubali kufungwa 1-0 na wageni wao Ruvu Shooting kutoka Mlandizi mkoani Pwani.

Kwa Upande wa Namungo FC mambo yaliwaendea Kombo baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 wakiwa nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa, ambao wanautumia katika kipindi hiki kufuatia Uwanja wao wa Majaliwa kuwa kwenye maboresho.

Msimu Mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara utaendelea tena hii leo Jumanne (Agosti 16) kwa michezo miwili, ambapo Singida Big Stars itakua nyumbani mjini Singida katika Uwanja wa Liti kuikaribisha Tanzania Prisons, iliyofunga safari kutoka jijini Mbeya.

Mchezo huu wa Ligi Kuu wa kwanza Msimu huu kuchezwa mjini Singida, utaanza majira ya saa nane mchana.

Mjini Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Mabingwa watetezi Young Africans watakuwa wageni wa Maafande wa Jeshi la Polisi ‘Polisi Tanzania’ ambao wamelazimika kuhamia Uwanjani hapo kufuatia Uwanja wa Ushirika Moshi kufungiwa kwa muda na TFF kwa kukosa sifa sinazostahili.

Uzuri ni kwamba katika upande wa kubashiri kampuni bora ya kubashiri Tanzania Sokabet inakupa fursa kuweka bashiri zako katika michezo hii na mingine kabla ya mchezo kuanza na wakati mechi inaendelea
Cha zaidi ni kwamba Sokabet inakupa ushindi mara dufu ya dau utakalotumia kubashiri kutokana na uwepo wa odds kubwa zaidi ambazo zinaongeza ushindi wako , tembelea www.sokabet.co.tz au bonyeza 14935# kujisajili na kuweka bashiri zako sasa ili kufaidi ushindi wako.

Mbali na hapo Sokabet inatoa 100% kwa mtu atakayefanya wekezo kwa mara ya kwanza.
Yote haya na mengine mazuri ni ndani ya Sokabet, the best online casino company and sports betting in Tanzania.

Diara hatarini kuikosa Polisi Tanzania
Kenya: William Ruto Rais mteule, amshukuru Mungu