Kamati ya mashindano ya chama cha soka visiwani Zanzibar (ZFA) ipo katika maandalizi ya mwisho ya ligi kuu ya soka visiwani humo kwa msimu wa 2016/17 ambao umepangwa kuanza kutimua vumbi mwanzoni mwa mwezi ujao.

Katibu mkuu wa ZFA Kassim Hadji Saloum amesema kwa sasa kamati ya mashindano inakamilisha baadhi ya taratibu za mwisho ambazo zitatoa taswara tofauti ya mshike mshike wa ligi ya msimu huu, ambao bado utashuhudia ligi ikichezwa katika kanda ya Unguja na Pemba kabla ya kuingia kwenye hatua ya fainali.

Hata hivyo Kassim Hadji Saloum ametoa wito kwa wadau wa soka wa ndani na nje ya Zanzibar kujitokeza kwa ajili ya kudhamini ligi hiyo ambayo wakati mwingine imekua ikikosa msisimko kutokana na ukata wa fedha.

Wenger: Wachezaji Wa Kiafrika Wana Ubunifu Na Nguvu
Nape Atema Cheche, Atangaza Kiama Kwa Walanguzi Wa Kadi