Chelsea wameendelea na mwendo wao wa kusuasua katika Ligi Kuu ya England kwa kukubali sare ya mabao 2-2 dhidi ya West Bromwich Albion.
Mabingwa hao watetezi wakashuhudia kila bao lao la kuongoza katika kila kipindi likirejeshwa kwenye uwanja wao Stamford Bridge.
Mabao Chelsea yalifungwa na César Azpilicueta dakika ya 20 na Gareth McAuley, beki wa West Brom aliyejifunga dakika ya 73.
Kwa upande wa West Brom mabao yao yalifungwa Craig Gardner katika dakika ya 33 na James McClean dakika ya 86.
Matokeo kamili ya mechi zilizochezwa Jumatano usiku:
Man City 0 – 0 Everton
Southampton 2 – 0 Watford
Stoke 3 – 1 Norwich
Swansea 2 – 4 Sunderland
Liverpool 3 – 3 Arsenal
Tottenham 0 – 1 Leicester