Raundi ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya inaanza kuunguruma leo majira ya saa 4:45 usiku kwa michezo miwili kuchezwa.

FC Basel watakuwa nyumbani kwao kuwakaribisha vinara wa Ligi Kuu soka England, Manchester City, wakati Juventus watakuwa na kibarua kizito dhidi ya Tottenham Hotspur.

Ligi hiyo itaendelea kesho Jumatano Februari 14 ambapo FC Porto ya Ureno itacheza na Majogoo wa jiji, Liverpool, huku mabingwa watetezi Real Madrid wakiwa kibaruani kupepetana na Paris Saint Germain.

Hatua hiyo itaendelea wiki ijayo ambapo Jumanne ya Februari 20, Bayern Munich itakuwa mwenyeji wa Besiktas huku Barcelona ikiwafuata Chelsea jijini London Uingereza.

Jumatano ya Februari 21, Manchester United itawafuata Sevilla wakati Shaktar Donetsk ikiumana na AS Roma.

Simba yaifuata Mwadui FC
Rabiot afunguka linalomkera PSG

Comments

comments