Ligi ya klabu bingwa barani Ulaya imeanza usiku wa kuamkia leo, ambapo jumla ya michezo saba kwenye makundi matano ilipigwa kwenye viwanja tofauti. Kundi A Basel ya nchini Uswiz ilitoka suluhu ya 1-1 dhidi ya Ludogorets Razgrad ya nchini Bulgaria.
PSG ikiwa nyumbani ililazimiswa sare ya bao 1-1 dhidi ya washika bunduki wa London Arsenal, huku PSG wakitangulia kupata goli la mapema sekunde ya 30 ya mchezo kupitia mshambuliaji wake Edinson Cavani, huku Goli la kusawazisha kwa upande wa Arsenal lilifungwa na Alexis Sanchez dk ya 78.
Tukio kubwa katika mchezo huo ni kadi mbili nyekundu zilizotolewa kwa timu zote mbili, Olivier Geroud alipewa kadi nyekundu dk ya 90 ya mchezo baada ya kadi ya njano aliyopewa dk ya 88, kwa upande wa PSG Marco Verratti nae alipata kadi nyekundu dakika ya 90 baada ya kadi ya njano aliyopewa dk ya 8
Lakini matokeo makubwa yalikuwa huko Barcelona baada ya kuibamiza Celtic idadi ya magoli 7-0 Messi akianza na hat- trick, magoli mengine yalifungwa na Suarez ambaye alipachika magoli mawili, Neymar na Iniesta wakipata goli moja moja, huku Mousa Dembele akikosa mkwaju wa Penalti kwa upande wa Celtic
Mchezo mwingine wa kundi D Bayern Munich iliicharaza FC Rostov ya nchini Urusi Magoli 5-0 huku Atletico Madrid ya nchini Hispania ikiwa ugenini ikiibuka na ushindi mwembamba wa goli 1-0 dhidi ya mwenyeji wake PSV Eindhoven ya nchini uholanzi.