Baada ya kukaa takribani miezi 10 pasipo kuchezwa ligi kuu soka Zanzibar kanda ya Pemba, hatimae leo ligi hiyo itaanza rasmi kuchezwa kwa michezo miwili katika viwanja tofauti, ambapo wapinzani kutokea mji mmoja wa Wete, timu ya Al-Jazira iliyopanda daraja itacheza na timu kongwe ya Kizimbani kwenye dimba la FFU Finya.

Pambano jingine litasukumwa katika dimba la Gombani ambapo timu kongwe ya Jamhuri iliyoanzishwa mwaka 1953 itachuana na Chipukizi.

Jamhuri na Chipukizi zilikutana September 17, 2012 kwenye ligi kuu ya soka ya Grand Malt Zanzibar na majogoo ya Wete walikubali kichapo cha mabao 3-0 huku mabao mawili ya Chipukizi yakifungwa na mpachika mabao Faki Mwalim ambaye kwa sasa ametua ndani ya klabu ya KMKM.

Ikiwa ligi hiyo kwa upande wa Pemba, inaelekea kwenye michezo ya awali, kanda ya Unguja hii leo inaelekea katika michezo ya ukiongoni ambapo saa 10 za jioni watacheza Polisi na Kimbunga katika dimba la Amani.

Ligi kuu soka ya Zanzibar msimu huu imejumuisha timu 28, ukiitoa Malindi waliosusia kucheza ligi kwa madai ya kutoitambua kamati iliokuwa inasimamia ligi hiyo kwa kanda ya Unguja ambapo kuna timu 14 kanda ya Unguja na timu 14 kanda ya Pemba.

Wawakilishi wa Zanzibar katika michuano ya kimataifa msimu ujao (2016-2017) kwenye klabu bingwa pamoja na kombe la shirikisho barani Afrika, watapatikanwa kwenye hatua ya 8 bora ambapo zitajumuishwa timu 4 za juu zilizomaliza kanda ya Unguja, na timu za kileleni zilizomalizia Kanda ya Pemba, na timu 2 za juu kwenye hatua hiyo ndizo zitakazokuwa bingwa na makamu bingwa wa ligi kuu soka Zanzibar.

Nini hatma ya timu ya Malindi ambayo ndio timu pekee iliyosusia kucheza ligi kanda ya Unguja?.

Wengi wanajiuliza vipi hatma ya Malindi yeye hajacheza ligi kuu pekeake kanda ya Unguja?.

Itashushwa daraja?, au watavuka maji kwenda kucheza kanda ya Pemba?, ambapo huko ndio kwanza lesho wanaanza ligi.

Jawabu lake ni rahisi mno, kwa mujibu wa taarifa za ndani kabisa zilizojificha kuwa timu ya Malindi itasubiri msimu ujao wa mwaka 2016-2017 na itacheza ligi kuu kama kawaida kuungana na wenzake.

Je msimu ujao kutakuwa na timu ngapi?.

Na timu ngapi zatashuka daraja?.

Awali kabla ya kutokea kwa vurugu la soka la Zenj kupelekwa Mahakamani, ni timu 3 za mwisho kwa kila kanda zitashuka daraja, lakini kwa taarifa za chini ya kapeti pengine huwenda isishuke hata timu moja daraja kwenye ligi hiyo na jambo hilo litapelekea msimu ujao ligi kuu soka ya Zenj kuwa na jumla ya timu 35 ambapo kanda ya Unguja itakuwa na timu 18 na kanda ya Pemba kutakuwa na timu 17 kwasababu msimu huu kwa jumla zipo timu 29 na pengine hakuna kushuka daraja wakati kupanda zitapanda timu 3 kwa kila kanda.

Ratiba Ya Nusu Fainali Ya FA Kupangwa Leo
Leicester City Hawakamatiki, Waendelea Kujichimbia Kileleni