Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali amesema, TAKUKURU ina taarifa zote za matumizi ya fedha za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), hivyo viongozi na wabunge wanapaswa kueleza ukweli wa kile wanachokijua.

Huvi karibuni Mbunge huyo ameomba kuhamia CCM mara baada ya Bunge la 11 kuvunjwa na ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi mara baada ya kutoka kuhojiwa na TAKUKURU.

Lijualikali ambaye ameingia katika mahojiano saa 2:20 asubuhi na kutoka saa 5:5 asubuhi amesema,wahojiwa wasiwe na hofu kwani mahojiano ni ya kirafiki na hakuna kitu kipya zaidi ya wanachokijua.

”Nlipokea wito kimsingi mahojiano yalikuwa ya kirafiki hakuna kitu kipya ,naomba nitoe ombi kwa wenzangu wote wanoendelea kuitwa kwaajili ya kuhojiwa waseme ukweli tu TAKUKURU wamejipanga na wanakila information wanakuja kuthibitisha, kama unahisi unaweza kudanganya huwezi kufanya hivyo maana hapa hatumsingizii mtu wala hatudanyanyi Umma” amesema Lijiualikali

Hata hivyo amewaasa wahojiwa wote kueleza ukweli wa kile wanachokijua kwani hata wakidanganya haitasaidia kitu.

Kocha Sven awatumia salamu Ruvu Shooting
Mdee na Bulaya watua Takukuru