Lil Kim bado hajamalizana kabisa na Nicki Minaj na popote jina lake linapotajwa haachi kumuweka kwenye kivuli cha kutompa heshima.

Katika mahojiano yake aliyofanya na Entertainment Tonight alipokuwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Paris Hilton iliyofanyika Magharibi mwa Hollywood, Lil Kim alidai kuwa hamjui Nicki Minaj baada ya kutakiwa kutoa maoni yake kuhusu rapa Cardi B na Nicki Minaj.

“Unajua, Cardi ni msichana wangu! Simjui huyo mwingine [Nicki Minaj]. Lakini Cardi ni mtu wangu na ninafurahi kwa sababu ya msichana wangu Cardi. Nashindwa kuvumilia kusubiri apate mtoto. Nakupenda, Cardi!,” alisema Lil Kim.

Mwaka 2011, uhasimu kati ya Nicki Minaj na Lil Kim ulichochewa na alichokisema Lil Kim alipofanya mahojiano na kipindi cha The Breakfast Club. Alisema kuwa hamheshimu Nicki Minaj kwa sababu ameingia kwenye muziki ‘akikopi’ mtindo wake wa kurap.

“Sijawahi kuwa na tatizo naye. Nilikuwa mtu mwema kwake. Alikuwa mtu mwenye maudhi,” alisema.

Rapa huyo aliyewahi kufanya kazi na B.IG alianza kurusha makombora yake kwa Nicki Minaji kupitia ‘Black Friday’ lakini Nicki Minaj alijibu pia kwa ngoma kadhaa ikiwa ni pamoja na ‘Stupid H*e’, ‘I am Your Leader’ na Roman’s Revenge’.

Black Friday ya Lil Kim na Pink Friday ya Nicki Minaj ziligeuka gumzo na kuchochea uhasimu kwa wasanii hao wa kike.

Kiwango cha Rakitic chaivutia Man Utd
Mke wa Waziri Mkuu Israel ashtakiwa kwa ufisadi