Rapa mkongwe wa kike, Lil Kim ametangaza tarehe ya kuachia albam yake mpya inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wake.

Malkia huyo wa michano ameitaja Mei 17 kuwa ndiyo siku atakayowapa mashabiki wake albam yake ya tano aliyoibatiza jina la ‘Nine’.

Novemba 2017, Lil Kim alitangaza kwa mara ya kwanza kuwa anaandaa albam ya ‘Nine’ ambayo ingetoka mwaka huu. Hivyo, ameamua kutekeleza ahadi yake bila kuchelewa.

“Nikiwa hapa, Mei 17, mtapata albam ya ‘Nine’ (9),” Kim aliwaambia mashabiki waliohudhuria tamasha lake huko Atlantic City. “Ni albam yangu ya tano. Nina mawe mengi kwa ajili yenu,” aliongeza.

Jina la albam hiyo limebeba maana nzito, kwa kuanzia tu, baba yake katika muziki, marehemu Notorious B.I.G aliuawa tarehe 9, Machi mwaka 1997. Juni 9 mwanaye Royal Reig alizaliwa, lakini pia albam hii ni mradi wake wa 9 ikiwa ni albam ya tano na ana mixtape (kandamseto) nne.

Alipofanya mahojiano na Hot 97 mwezi uliopita, Kim alitangaza tena jina la albam hiyo ambayo inakuwa ya kwanza kusikika tangu mwaka 2005 alipoachia ‘Naked Truth (Ukweli mtupu’.

Jafo ahimiza ushirikiano na WFP
Mahakama ya Rufaa yapendekeza umri wa kufanya ngono kuwa miaka 16

Comments

comments