Rapa wa Marekani Lil Wayne amedai kuwa anahisi yeye ni raia wa Nigeria angalau kwa asilimia 53, kutokana na programu ya kutambua uhalisia aliyoitumia.

Mkali huyo wa ‘6-foot 7 foot’, amefunguka kwenye mahojiano aliyofanya na DJ EFN na N.O.R.E kwenye kipindi cha ‘Drink Champ’ ha Revolt TV, baada ya kuulizwa kwanini aliitaja Nigeria kwenye moja kati ya nyimbo zake kali.

“Naipa tano Nigeria, nilifanya mahojiano/usaili kwenye ancentry.com kuhusu ‘My23 and Me’ na matokeo yalikuja kama 53% ni raia wa Nigeria. Yeah, sasa mimi na mama yangu tunatakiwa kukaa tujadili kidogo (akacheka),” alisema Lil Wayne.

‘My 23 and Me’ inafanywa zaidi na mtandao wa Ancestry.com ambao unahusisha zaidi kutafuta asili ya mtu miaka takribani 500 iliyopita, kwa kutumia program ya kompyuta ambapo inaweza kukupa matokeo ya kuwa na asili ya nchi kadhaa kwa asilimia.

Wiki iliyopita, Lil Wayne ambaye jina lake halisi ni Dwayne Michael Carter Jr. aliulizwa sehemu mbili ambazo anatamani kuzitembelea duniani, alitaja Nigeria na Misri.

Huenda Nigeria ikabarikiwa kutembelea na mshindi huyo wa tuzo nne za Grammy mwenye rekodi ya kuuza muziki wake kwa jumla ya zaidi ya nakala milioni 100 duniani kote ikiwa ni pamoja na nakala milioni 15 za albam zake; na zaidi ya nakala milioni 37 ya nyimbo zake kwa njia ya mtandao nchini Marekani pekee.

Raia wa Nigeria wametumia mitandao ya kijamii kuendelea kumshawishi Lil Wayne atue nchini humo, wakimuita ‘kaka, ndugu yetu’, wakimkaribisha nyumbani.

Membe alivyowasili kwenye Kamati ya CCM kuhojiwa
Video: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Februari 6, 2020

Comments

comments