Lil Wayne amewapa sababu ya kutabasamu mashabiki wake huku ikiwa mwiba kwa mahasimu wake baada ya kutoa tangazo jipya la albam yake inayosubiriwa kwa hamu ya ‘The Carter V’ iliyosubiriwa kwa miaka kadhaa sasa.

Akitema cheche za mistari juu ya jukwaa la Story nightclub iliyoko Miami, Weezy aliweka nukta kidogo na kuwaambia mashabiki wake kuwa amefanya kikao muhimu kuhusu mpango wa kuachia albam hiyo, hali iliyozua shangwe.

“Ninataka tu kuwafahamisha nilikuwa na kikao leo,” alisema. “Kilikuwa kikao kirefu. Wote mfahamu, kikao kilikuwa cha kuchagua tarehe ya kuachia rasmi ‘Tha Carter V’.

Mapema mwezi huu, mahakama ilimaliza mgororo uliochelewesha kuachiwa kwa albam hiyo uliodumu kwa muda mrefu kati ya Cash Money Records na rapa huyo. Kutokana na uamuzi wa kisheria, Weezy aliachana rasmi na lebo hiyo, lakini bado lebo hiyo itasimamia kuachiwa kwa albam yake kupitia Universal Music Group.

The Carter V imechelewa tangu ilipotangazwa kwa mara ya kwanza mwaka 2012. Hata hivyo, wakati akisubiri kutatua mgogoro uliyohusisha albam hiyo, Lil Wayne aliendelea kuachia miradi isiyo rasmi kama kanda mseto ya Dedication 6.

Majuto yupo hai, taarifa ya kifo chake ipuuzwe
Jumla ya walipakodi 676 Njombe wasajiliwa TRA

Comments

comments