Mtangazaji maarufu wa kipindi cha The Playlist Times FM, Omary Tambwe ‘Lil Ommy’ amekuwa moja ya watu wachache duniani kupokea Tuzo maalum ya Pongezi kutoka Makao Makuu ya YouTube, Marekani.

Lil Ommy amepokea tuzo ya YouTube Play Button Silver Metal yenye madini ya Silva kutoka Marekani YouTube na kusainiwa na CEO wa YouTube, Susan baada ya channel yake ya YouTube kufikisha Subscribers laki moja (100K).

Tuzo hizo hutolewa na mtandao wa YouTube kwa watengenezaji wa maudhi kwenye mtandao huo (YouTube Creators) ambao wanafanya vizuri, wana content nzuri zinazotazamwa sana na kufuatiliwa zaidi na ambazo huingia mpaka kwenye trending.

Watu wenye Subscribers laki hupewa tuzo yenye madini ya Silver na wanaofikisha million moja hupewa ya dhahabu (Gold) na wale wenye kufikisha million 10 wanapewa ya almasi (Diamond) bila kupigiwa kura wala kushindanishwa kwa kuwa YouTube wenyewe wanaangalia performance au mwenendo wa watu wanaoweka vitu kwenye mtandao huo kama zinavutia watazamaji na bila kuvunja sheria na kanuni za mtandao huo na mambo mengine.

Huu ni ujumbe ambao aliandikiwa Lil Ommy kwenye barua iliyosainiwa na CEO wa YouTube, Susan ambayo iliambata na tuzo hiyo iliyotumwa April 13 na kufika Tanzania April 18.

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Aprili 22, 2018
Makonda aja na mradi mwingine kwa kina baba