Mshambuliaji mahiri wa vinara wa ligi ya Hispania FC Barcelona Lionel Messi, amempa ushauri Neymar kwa kumtaka asikubali kujiunga na klabu ya Real Madrid ambayo inatajwa kuwa katika harakati za kumsajili itakapofika mwishoni mwa msimu huu.

Messi amemtumia salamu hizo Neymar, huku akimwambia ni vyema akajiunga na Manchester City ya England, kwa kuwa anatambua huko atakua na maisha mazuri zaidi kuliko Hispania, tena akiwa na timu pinzani na aliyowahi kuitumikia nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa na jarida Don Balon ambalo limeandika taarifa za mshambuliaji huyo kumshauri Naymar, zinaeleza kwamba harakati hizo za Messi ni kutaka kumuunganisha mchezaji huyo wa kibrazil na Pep Guardiola ambaye kwa sasa ndio mkuu wa benchi la ufundi huko Etihad Stadium.

Messi ameliambia jarida hilo kuwa, anaamini Neymar atakua mwenye furaha zaidi kama atakua chini ya meneja Guardiola, kutokana na kumtambua vilivyo, huku akiwakandia Real Madrid kwa kusema hawatoweza kumtunzia kipaji chake ipasavyo.

Neymar, mwenye umri wa miaka 26, alisajiliwa na Paris Saint-Germain mwishoni mwa msimu uliopita kwa ada iliyovunja rekiodi ya dunia ya Pauni milioni 198, na amekua akihusishwa na taarifa za kutaka kundoka jijini Paris na kumtikia kwingineko.

Video: Ujio mpya wa Ney wa Mitego ''Amsha Popo"
Simba Vs Young Africans kumaliza ubishi April 29

Comments

comments