Mshambuliaji nyoita wa Barcelona, Lionel Messi ameonyesha mapenzi makubwa kwa nyota mwingine wa zamani wa timu hiyo, Ronaldinho.

Messi amechukua jezi yake namba 10 na kuandika ujumbe mzuri wa kuonyesha shukurani kwa Ronaldinho ambaye walicheza wote Barcelona katika timu kubwa kuanzia mwaka 2004 hadi 2008.

Wakati huo Ronaldinho ndiye alikuwa mchezaji nyota zaidi na Messi ameonyesha kufurahishwa na namna Mbrazil huyo alivyomuunga mkono wakati akikua kisoka wakati akipanda timu ya wakubwa akiwa na miaka 16.

Baadaye kupitia mtandao wa Instagram, Ronaldinho ,36, alionyesha kuwa ameipokea jezi hiyo kama zawadi bora kabisa kwake. Ronaldinho ndiye aliyemrithisha Messi jezi namba 10.

Donald Trump Achafua Hewa, Ataka Waislamu Wasiingie Marekani
Mayweather Aonyesha Anavyoponda Raha