Mshambuliaji wa kutumainiwa wa FC Barcelona Lionel Messi, ameonyesha kuwa na matumaini makubwa na meneja Pep Guardiola kushinda mtihani wa kukibalisha kikosi cha Man City na kuwa na ubora kimataifa.

Messi ameonyesha matumaini hayo ikiwa ni baada ya siku kadhaa kupita ambapo kikosi cha Barcelona kiliibanjua Man City jumla ya mabao manne kwa sifuri katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Messi ameliambia gazeti la The Sun: “Man City ni klabu kubwa na ina kikosi cha ushindani. Wameendelea kuwa klabu yeney suhindani katika kila mwaka, lakini kwa ujio wa Guardiola ninaamini ubora wao utaendelea kuimarika zaidi.

“Licha ya matarajio yangu kuwa katika mipango ya muda mrefu, lakini hata hivi sasa kikosi cha Man City ni kizuri na kinaweza kupambana na yoyote katika soka la hapa Ulaya na kwingineko duniani.”

Kuhusu mshambuliaji mwenzake kutoka nchini Argentina Sergio Aguero, Messi ameongeza kuwa: “Kun ni mtu mwenye uelewa wa kutosha na wakati mwingine ni vigumu kumfanyia tathmini katika maamuzi yake, lakini naamini ni mchezaji mzuri na atafanikiwa kuendelea kuwa sambamba na Guardiola licha ya kuwepo kwa tetesi za kutaka kuondoka.

“Miongoni mwa wachezaji ambao nina imani wataweza kufanikisha ubora wa Man City chini ya Guardiola ni Kun, hivyo sina shaka nae kuhusu kubaki klabuni hapo.” Aliongeza Messi

Video: DC mjema autaja mkakati wake kuhusu machinga Ilala
Issa Hayatou Amshika Mkono Jamal Malinzi CAF