Mshambuliaji na Nahodha wa Kikosi cha Argentina Lionel Messi amesema Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka huu huenda zikawa za mwisho katika kutimiza ndoto yake ya kushinda Ubingwa wa Michuano hiyo.

Mshambuliaji huyo wa Mabingwa wa Ufaransa Klabu ya Paris Saint-Germain ameshacheza Fainali nne za Kombe la Dunia, akikaribia kuywaa ubingwa 2014 wakati Argentina ilipobamizwa bao 1-0 na Ujerumani nchini Brazil.

Amesema yupo tayari kwa fainali za mwaka huu na amedhamiria kupambana kwa kushikiana na wenzake, ili kufanikisha lengo analolikusudia kama mchezaji na kisha kutimiza lengo timu nzima kwa ujumla.
“Huu ni wakati maalum, uwezekano mkubwa wa Fainali zangu za mwisho,”

“Nafasi yangu ya mwisho ya kutimiza ndoto yangu binafsi, na ndoto yetu kama timu ya Taifa ya Argentina, kuwa ukweli.”

Argentina ni miongoni mwa wanaopewa nafasi kubwa ya kunyanyua kombe hilo pamoja na wapinzani wa Amerika Kusini Brazil.

Walakini, nafasi nyingi za Argentina zitakuwa kwa Messi, ambaye amekuwa katika kiwango bora msimu huu kwa PSG.

“Ninajisikia vizuri sana, niko vizuri,” alisema Messi.

“Nadhani nimekuja hapa nikiwa na tayari kupambana. Sina wasiwasi wowote. Nina uhakika kila mmoja wetu yupo tayari kupambania timu ili ipate matokeo mazuri.”

“Tuko katikati ya msimu na ninajihisi vizuri. Tukianza kucheza michezo mingine michache, tutapata kasi na nimetoka kucheza katika klabu yangu ya PSG. kwa hiyo nipo FIT kwa lolotekatika Fainali hizi za Kombe la Dunia.”

“Sijafanya chochote tofauti, nilijitunza tu.” amesema Messi kabla ya mchezo wa kwanza ya Kundi C dhidi ya Saudi Arabia utakaopigwa saa saba mchana leo Jumanne (Novemba 22).

Hadi sasa Lionel Messi ameshafunga mabao 12 na asisti 14 katika michezo 19 aliyoichezea PSG msimu huu katika mashindano yote.

Pia amekuwa katika kiwango kizuri kwa Argentina, akifunga mabao 10 katika michezo iliopita na kutoa mchango wa mabao mengi katika michezo mitano mfululizo.

Messi kwa sasa ana umri wa miaka 34, na ikitokea anaendelea kuwa katika kiwango cha kucheza soka la ushindani katika Fainali zaijazo za Kombela Dunia mwaka 2026, atakua na Umri wa miaka 38, hivyo mwaka huu amedhamiria kukamilisha ndoto ya kutwaa Ubingwa wa Michuano hiyo.

Hata hivyo Argentina inatajwa kuwa miongoni mwa mataifa yanayotabiriwa kutwaa ubingwa wa Fainali za Mwaka huu Qatar, na kama itatokea, bado Gwiji huyo atakua amefanisha lengo lake.

Mashabiki Ufaransa washushwa PRESHA
Rais kuzindua Bunge na hotuba hali ya nchi