Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi ameonyesha dalili kwamba yu tayari kucheza mchezo wa mahasimu kati ya Barcelona na Real Madrid utakaopigwa Jumamosi hii baada ya kuonyesha rasmi viatu vyake vipya.

Nyota huyo ameonyesha viatu maalum vilivyotengenezwa na kampuni ya Adidas kwa ajili ya mchezo wa ‘EL Classico’ siku ya Jumamosi.

                                                           Viatu hivyo vimepambwa na rangi nyeusi,kijani na nyekundu.

Messi hajacheza mchezo wowote tangu alipoumia katika mchezo dhidi ya Las Palmas mnamo mwezi wa tisa mwaka huu jambo ambalo linawapa wasiwasi Barcelona kwamba huenda akaukosa mchezo wa Jumamosi.

Messi alionekana juzi katika viwanja vya mazoezi vya klabu ya Barcelona akifanya mazoezi na taarifa za kitabibu toka klabu ya Barcelona zinasema kuwa nyota huyo anaweza kucheza mechi hiyo ingawa ni mapema kuwa na uhakika wa asilimia 100.

Mkwasa Awashukuru Watanzania Kwa Kuwapa Somo
Kocha Wa Soka Aukwaa Uwaziri Mkuu