Mshambuliaji na nahodha msaidizi wa FC Barcelona Lionel Andres Leo Messi huenda akajumuika na wenzake katika mchezao wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Deportivo La Coruna.

Messi alipatwa na majeraha ya misuli ya mapaja majuma mawili yaliyopita, hali  ambayo iliibua hofu miongoni mwa wachezaji wenzake pamoja na kwa mashabiki wa FC Barcelona kufuatia taarifa kueleza kuwa, huenda ingemchukua muda wa majuma manne kujiuguza.

Jioni hii taarifa kutoka Camp Nou zinaeleza kuwa, mshambuliaji huyo ambaye ametwaa tuzo ya mchezaji bora mara tano yupo katika hali nzuri baada ya kuanza mazoezi mepesi chini ya uangalizi wa matabibu wa FC Barcelona.

Hata hivyo inaelezwa kuwa, endapo atashindwa kucheza mchezo wa ligi ya nchini Hispania mwishoni mwa juma hili, Messi huenda akawa fit kwa ajili ya mpambano wa ligi ya mabingwa barani Ulaya ambao utaikutanisha FC Barcelona Dhidi ya Manchester City kati kati ya juma lijalo kwenye uwanja wa Nou Camp.

Mchezo huo utakua unamrejesha nyumbani kwa mara ya kwanza meneja wa Pep Guardiola tangu alipotangazwa kuchukua nafasi ya umeneja huko Etihad Stadium.

Gari la kwanza kutengenezwa na kampuni ya Kitanzania kuzinduliwa Desemba 2016
Rais Magufuli apokea hati za utambulisho za Balozi wa Sudan, Slovakia, Ukraine na Ghana