Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi yupo kwenye mashaka ya kukosa mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu huu wa 2016/17, ambao utashuhudia FC Barcelona wakipapatuana na Celtic kati kati ya juma lijalo.

Messi alipatwa na majeraha ya paja akiwa na timu ya timu ya taifa ya Argentina ambayo alitangaza kuachana nayo mara baada ya fainali za Copa America zilizofanyika mieizi mitatu iliyopita nchini Marekani, lakini baadae alitengua maamuzi yake na kukubali wito wa kocha mpya Edgardo Bauza.

Mwishoni mwa juma lililopita Argentina ilipambana na timu ya taifa ya Uruguay katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018, na Messi alifunga bao pekee lililoipa ushindi timu yake ya taifa.

Hii leo Argentina inatarajiwa kuingia uwanjani kupambana na timu ya taifa ya Venezuela bila ya kuwa na Lionel Messi, ambaye ameripotiwa kurejea mjini Barcelona kwa ajili ya kuanza matibabu ya misuli ya paja.

FC Barcelona wametoa taarifa za maendeleo ya mshambuliaji huyo, ambazo zinaeleza hatokua sehemu ya kikosi cha mwishoni mwa juma hili, ambapo mabingwa hao wa Hispania watapambana na Alaves.

Taarifa hizo zimeongeza mashaka kwa mashabiki wa FC Barcelona, kufuatia wasiwazi wa kukosekana kwa Lionel Messi kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Celtic.

Jopo la madaktari linalomshughulikia Messi, limeonyesha kuwa na wasiwasi wa mchezaji huyo kuwa fit kabla ya mchezo huo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya utakaochezwa siku ya jumanne, hivyo meneja wa Barcelona Luis Enrique ameshauriwa kuwa mtulivu kwa sasa.

Video: Kamanda Sirro akionyesha silaha za kivita zilizokamatwa
Furaha Ya Kufuzu Kwa AFCON 2017, Itakua Chungu Kwa Klabu Za Ulaya