Mwanasiasa mkongwe, Profesa Ibrahim Lipumba ameendelea kukosoa uteuzi wa Profesa Sospeter Muhongo kurudi katika wizara ya Nishati na Madini aliyokuwa akiishikilia kabla ya kujiuzulu kufuatia kashfa ya Escrow katika serikali ya awamu ya nne.

Profesa Lipumba ambaye hivi karibuni alieleza kuwa kuteuliwa kwa Profesa mwenzake Muhongo hakuko sahihi kwa kuwa bunge liliazimia aondolewe katika nafasi yake hiyo baada ya kumhoji kutaweza kuzua utata mkubwa husasan pale suala la Escrow litakapoendelea kutumbuliwa kama jipu, ameibuka na jingine.

Akizungumza leo katika kipindi maalum cha Azam TV, Lipumba amedai kuwa mbali na kashfa hiyo, Profesa Muhongo sio mwanasiasa anayezingatia mahusiano ya umma (Public Relations).

“Profesa Muhongo hana public relations, hata mwaka 2013 aliwahi kutoa hotuba uko kusini baada ya hapo watu wakaandamana,”alisema Profesa Lipumba.

Huyu Ndiye Rapa Mwenye Asili ya Tanzania Aliyetajwa Tuzo za Grammy
Roger Federer Kucheza Na Martina Hingis