Profesa Ibrahim Lipumba ameendelea kueleza msimamo wake dhidi ya aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema akiungwa mkono na vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa, Edward Lowassa.

Akizungumza jana kwenye ofisi za makao makuu ya CUF jijini Dar es Salaam, Profesa Lipumba alisema kuwa aliamua kujiuzulu uenyekiti wa chama hicho baada ya nafsi yake kumsuta kwa kuwa alikuwa anamfahamu Lowassa ambaye alisoma naye Chuo Kikuu japo alikuwa mwaka mmoja nyuma yake.

Alisema asingeweza kumpigia debe Lowassa kwa sababu aliwahi kuwa mwanachama wake wakati Profesa akiwa ndiye mwenyekiti wa  Tanu Youth League ambayo sasa ni UVCCM.

“Nilisema siwezi kuwa mpiga debe wa Lowassa. Mimi ni Profesa, Lowassa alikuwa mwaka mmoja nyuma yangu pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alikuwa anafanya shahada ya sanaa,” alisema Profesa Lipumba.

“Mimi niliokuwa nilikuwa Mwenyekiti wa Tanu Youth League ambayo sasa hivi ni UVCCM, alikuwa mwanachama wangu, kwa hiyo namfahamu siku nyingi,” aliongeza.

Katika hatua nyingine, Lipumba alieleza kuwa hawezi kushiriki mkutano wa Baraza Kuu la chama hicho unaofanyika leo visiwani Zanzibar kwa kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye ndiye anayepaswa kuuandaa hayupo nchini.

Hata hivyo, Maalim Seif alirejea jana hivyo kushiriki kikao hicho ambacho Lipumba anayeendelea kudai kuwa mwenyekiti halali wa CUF amedai hakitambui.

Majimaji FC Wamrejesha Kally Ongala
Diamond ampooza Zari, Ijue gharama ya nyumba aliyomzawadia kwenye birthday yake