Mwanasiasa Mkongwe, Profesa Ibrahim Lipumba ameweka wazi namna ambavyo rais John Magufuli alisaidia kuiondoa mahakamani kesi ya kuandamana bila kibali iliyokuwa inamkabili.

Profesaa Lipumba na wanachama wengine wa Chama Cha Wananchi (CUF), walikuwa wakikabiliwa na kesi ya kufanya mkusanyiko na maandamano bila kibali wakati mwanasiasa huyo mkongwe alipokuwa Mwenyekiti wa chama hicho, kesi iliyoendelea kuunguruma hata baada ya kujiuzulu nafasi yake ya uenyekiti.

Akizungumza jana katika kipindi maalum cha Azam TV, Profesa Lipumba alieleza kuwa rais Magufuli alimuita Ikulu jijini Dar es Salaam na kumueleza kuwa hakupenda kuendelea kwa kesi hiyo mahakamani na kwamba alikuwa na mpango wa kuagiza serikali iiondoe.

“Kwahiyo alikuwa anahitaji kuifuta ikiwa mimi mwenyewe naridhika, maana yake isije ikawa kama nahitaji kesi iendelee mahakamani. Mimi nikasema ‘kweli hii mimi inanisumbua, huwezi kupanga mipango yako na sina kosa lolote nililolitenda’,” Profesa Lipumba alisimulia.

Mwanasiasa huyo alimsifu rais Magufuli kwa kuwa mtu anayefanyia kazi maneno yake ndani ya muda mfupi.

“Ilikuwa Jumatatu, mara Alhamisi naitwa kule naambiwa serikali imeamua kuiondoa kesi mahakamani,” aliongeza.

Haki za Binadamu, Utawala Bora Yalaani Hatua za Wakuu wa Wilaya Kuwatupa Selo Watumishi
Sumaye Akosoa Uamuzi Wa Rais Magufuli Kuhusu Wakwepa Kodi