Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba, anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, amesema kuwa yupo tayari kukaa meza moja na Maalim Seif ili waweza kumaliza tofauti zilizojitokeza.

Lipumba amesema kuwa inashangaza kwa sasa hazungumzi na Katibu Mkuu wa chama hicho ambaye wanafahamiana kwa zaidi ya miaka 40 sasa.

Amesema kuwa amekuwa karibu na maalim Seif tangu mwaka 1973 wakiwa chuo kikuu cha Dar es salaam(UDSM), hivyo inamsikitisha kuona inafikia hatua hiyo.

“Kusema ukweli ningependa kurejea kwenye mazungumzo ili kuendelea kujenga chama mimi namtambua Maalim Seif ndiye katibu wetu namhitaji aje tufanye kazi, ofisi yake ipo ila leo imefikia hata simu yangu hapokefi inaniuma sana,”amesema Lipumba.

Aidha Lipumba amesema kuwa shutuma za kwamba analindwa na Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini si za kweli,kwani wajumbe wa mkutano mkuu wa chama ndio waliopeleka barua kwa Msajili kupata tafsiri ya ya katiba kutokana na hatua zilizofanyika katika mkutano mkuu.

Waalimu wakimbia uhakiki wa vyeti
Nape amvaa Makonda kuhusu madawa ya kulevya kwa wasanii