Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amegoma kujisalimisha kwa Jeshi la Polisi kufuatia amri ya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutaka akamatwe kwa kushindwa kuhudhuria kesi yake mahakamani hapo bila kutoa taarifa.

Lissu amedai kuwa hatajisalimisha polisi kwani hajapata barua ya mahakama au polisi inayomtaka afanye hivyo na kwamba hawezi kuchukua hatua kwa kusikiliza kinachosemwa kwenye vyombo vya habari.

“Mimi siwezi kufanyia kazi habari za magazeti katika masuala ya kisheria, nipo hapa ninaendelea na shughuli zangu kama kawaida na kama mnavyoniona niko katika kuwawakilisha wananchi wa jimbo langu,” alisema Lissu.

Hakimu Thomas Simba ambaye alitoa agizo hilo, alisema Lissu haudhurii kartini kusikiliza kesi ya uchochezi inayomkabili yeye na wahariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina na Jabir Idrisa na Ismail Mehboob ambaye ni mchapishaji wa gazeti hilo.

Mdhamini wa Lissu, Robert Katula aliiambia Mahakama kuwa alishindwa kufika mahakamani hapo kwakuwa alikuwa akihudhuria kesi ya uchaguzi katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza.

 

Joto la uchaguzi nchini Marekani lazidi kupanda
Asasi za Kiraia zaanzisha harakati kudai katiba mpya, zawatenga wanasiasa