Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika TLS, Tundu Lissu amesema kuwa watu waliomshambulia walikuwa wamedhamiria kufanya mauaji ya kisiasa.

Ameyasema hayo hii leo jijini Nairobi nchini Kenya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa mpaka sasa hakuna mtu wala kikundi kilichokamatwa kuhusu shambulio hilo.

Amesema kuwa mpaka sasa hawajahojiwa na hakuna tetesi zozote za kukamatwa kwa watuhumiwa ambao walitekeleza shambulizi hilo.

Aidha, ameongeza kuwa tangu ashambuliwe akiwa mjini Dodoma, Bunge halijapeleka hata senti tano kwa ajili ya matibabu anayopatiwa jijini Nairobi.

“Katika historia ya kisiasa na Bunge Tanzania, haijawahi kutokea kikundi cha watu kuchukua silaha kwa ajili ya kwenda kuua kiongozi kwa sababu tu anaongea mambo ambayo hawayapendi,”amesema Lissu

Hata hivyo, ameongeza kuwa bado kuna risasi moja mwilini mwake ambayo haina madhara na endapo watataka kuitoa ndipo itakaposababisha madhara makubwa.

Australia yapania kuwa muuzaji namba moja wa bangi duniani
Rugemalira awataja wezi wa Escrow