Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambaye anaendelea na matibabu nchini Kenya amesema kuwa wanaendelea kupigana na watashinda vita hiyo ya ukombozi wa Demokrasia.

Ameyasema hayo baada ya kukutana na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa CUF, Ismail Jusa Ladhu alipomtembelea jijini Nairobi.

“Leo nina furaha sana kwa kupata fursa ya kumtembelea sahib na ndugu yangu, Tundu Lissu, Nairobi Hospital anakoendelea kupata matibabu baada ya kupigwa risasi zipatazo 16 mwilini Septemba 7, mwaka huu, ametaka niwafikishie ujumbe huu,”amesema Jusa

Hata hivyo, Jussa amedai kuwa afya ya Tundu Lissu kwa sasa inaendelea vizuri sana, hivyo amewaasa watanzania kuendelea kumuombea.

NASA watoa jipya kuhusu mpango wa kumuapisha Raila Odinga
Zitto aonyesha kutoridhishwa na maamuzi ya JPM