Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika TLS, Tundu Lissu ameitaka mahakama kutopokea ushahidi vielezo wa vishungi vya bangi vilivyokutwa katika nyumba ya msanii wa bogo muvi, Wema Sepetu kwa madai kuwa vishungi hivyo ni sigara.

Lissu amepinga msokoto huo mmoja usipokelewe mahakamani kama kielelezo cha ushahidi kwani ndani ya bahasha iliyokamatwa kuna vitu zaidi ya msokoto mmoja na vipisi viwili vinavyodaiwa kuwa ni bangi.

“Mheshimiwa hakimu, vipisi viwili vyenye majani ukiviangalia kwa makini ni vishungi vya sigara ambayo imetumika kwa sababu vina alama ya kuungua, kwetu vinaitwa twagosoo, kitu kinachoitwa msokoto wa bangi havijulikani, haiwezekani vitu vilivyotolewa kwenye bahasha vikawa ni vielelezo vya ushahidi,”amesema Lissu

Aidha, Wema na wenzake Angelina Msigwa na Matrida Abbas wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa ambapo ni kinyume cha sheria.

Hata hivyo, Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Thomas Simba mara baada ya kusikiliza hoja hizo amesema kuwa mahakama itatoa uamuzi wa kupokea ama kutopokea  kielelezo hicho Agosti 18 mwaka huu.

 

Video: Lissu atinga kortini kumtetea Wema, Msako wa fedha za Ecsrow Ulaya balaa
Rais Edga Lungu: Kupima ukimwi si jambo la hiari