Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika TLS, Tundu Lissu amekamatwa na Jeshi la Polis jijini Dar es salaam akitokea mahakama ya Kisutu.

Mwanasheria huyo anayekabiliwa na kesi ya uchochezi lakini pia ni wakili wa mfanyabiashara, Yericko Nyerere ambapo mapema hii leo alikuwa mahakamani hapo kwaajili ya kutoa utetezi kwa mfanyabiashara huyo.

Hayo yamesemwa na Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene ambapo amesema kuwa wakati gari la Lissu likiwa liko getini tayari kwa kutoka mahakamani hapo, lilizuiwa na gari la Polisi likiwa na askari na kumtaka atelemke na kumuweka chini ya ulinzi huku wakimpeleka kituo cha polisi kati.

Hata hivyo, siku za hivi karibuni Mwanasheria huyo wa Chadema na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika TLS amekuwa akikabiliwa na tuhuma za uchochezi kitu ambacho kimekuwa kikizua mijadala mikubwa.

Marcelo Bielsa Kumrejesha Batshuayi Ufaransa
FC Barcelona Yaitega Tena Liverpool