Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amekana kuchapisaha taarifa za uchochezi zenye kichwa cha habari kisemacho: ‘Machafuko yaja Zanzibar’ kwa sababu yeye si mchapishaji.

Lissu amekana mashtaka hayo Mbele ya Hakimu Mkuu Thomas Simba wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam, wakati upande wa jamhuri ulipomsomea maelezo ya awali na wenzake kuhusu kesi ya uchochezi inayowakabili.

“Sikubali kama kulikuwa na uchaguzi halali wala Serikali halali Zanzibar, kwa sababu kitu hicho hakipo kisheria,”amesema Lissu.

Aidha, Lissu amekana kutisha na kuwatia hofu wananchi wa Zanzibar wasiingie kwenye uchaguzi wa marudio ya Uchaguzi Mkuu, huku wakili wa serikali, Patrick  Mwita akiendelea  kusoma maelezo hayo, Lissu alikubali jina lake,umri wake,kazi na makazi yake na kwamba ameshtakiwa kwa makosa yanayomkabili.

Kwa pamoja washtakiwa wote wanakabiliwa na mashtaka matano yakiwamo ya kuandika habari za uchochezi kinyume na sheria ya Magazeti ya Mwaka 2002.

 

Kafulila: Chadema hii ni ya mwendo kasi
Video: Vilio vinne kufungwa mgodi mkubwa nchini, Ubunge wa Bulembo na Kabudi shakani