Mbunge wa Singida Mashariki kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amesema kuwa hakuna ukweli wowote kuwa chama chake kimehusika na shambulio dhidi yake kwani nyumba ile ina ulinzi na walinzi wameajiriwa na serikali,

Amesema kuwa kama kuna mwenye uwezo wa kuondoa walinzi lindoni muda wa kazi bila kujua walikuwa wapi na kwanini basi ndio atakuwa amehusika na shambulio hilo.

“Nimekaa eneo lile kwa zaidi ya miaka 7, CCTV Camera zipo na walinzi wapo siku zote sasa Waziri anapokanusha hili atueleze, nini kimetokea na Camera imeng’olewa lini na nani?,” amehoji Lissu.

Aidha amesema kama Mbowe na CHADEMA wana uwezo wakuondoa Camera na walinzi katika eneo wanaloishi viongozi wa serikali basi watakuwa wamehusika wao, lakini hicho ni kitu ambacho hakiwezekani”.

Hata hivyo, Jana akizungumza jijini Arusha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema kuwa, Lissu ndiye mlalamikaji wa kesi, inakuwaje mwenye kesi naye mpaka tuanze kulazimishana ili aje, mwanzoni tulidhani ni mgonjwa akipata nafuu atakuja kwenye kesi yake, tunamshuhudia kapata nafuu kaanza uzembe na uzururaji tunamtaka Lissu arudi nchini”.

 

 

Wanafunzi walioongoza mtihani kidato cha nne watoa neno
Man Utd wataja hasara waliyoipata kwa kumtimua Mourinho