Mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, amesema kuwa marehemu Samuel Sitta ndiye aliyewahi kuwa Spika wa Bunge bora zaidi kwa kuwa aliruhusu wabunge kuongea.

Amesema hayo wakati akizungumza na wanachi wa Urambo mkoani Tabora, ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya kampeni kwa ajili ya uchaguzi mkuu Oktoba 28, 2020 katika maeneo mbalimbali nchini.

“Nyie mnafahamu mzee Sitta alikuwa ni mbunge hapa kwa miaka 30, Sitta alikuwa Spika wa Bunge, katika historia yetu ya kibunge hatujawahi kuwa na Spika wa aina kama marehemu Mzee Sitta, na sifa yake ni moja tu aliruhusu wabunge kusema kwa sababu ni mahali pa kusema”, amesema Lissu.

“Nataka tuwe watu huru, rais tunamchagua wenyewe akikosea tuwe na haki ya kumsema, mbunge akikosea tuwe na haki ya kumsema, Mkuu wa wilaya na Mkuu wa mkoa wakikosea tuwe na haki ya kuwakosoa kwa sababu hawa tunaambiwa ni watumishi wetu”. amesema Lissu.

Baraza la Mambo ya Nje UE hofu ya kuenea kwa Covid 19
Mwalimu auawa kwa kukatwa kichwa Ufaransa