Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ametolewa salama katika chumba cha upasuaji na kuhamishiwa katika chumba cha uangalizi maalumu mara baada ya kufanyiwa upasuaji huo.

Hayo yamesema na Mkuu wa Idara ya Uenezi ya Chadema, Hemedi Ali ambapo amesema kuwa upasuaji huo umefanyika kwa mafanikio makubwa hivyo yupo Executive ICU kwaajili ya uangalizi zaidi.

Aidha, Ali amesema kuwa madaktari wamewahakikishia kuwa hakuna tishio lolote la kiafya na anafahamu zote kitu ambacho amesema ilikua ni hatua ngumu kuifikia kwani alikuwa katika hatua mbaya.

Hata hivyo, ameongeza kuwa wataendelea kutoa taarifa kadri zinavyowafikia kutoka kwa madaktari wa hospitali aliyolazwa jijini Nairobi

Mane anyakua tuzo ya mchezaji bora wa mwezi
Video: IGP Sirro awatoa wasiwasi wazazi, anena mazito kuhusu Lissu