Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amesema kuwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, halijawahi kumlipia gharama za matibabu kutokana na majeraha aliyoyapata baada ya kushambuliwa na risasi Septemba mwaka juzi.

Hata hivyo, Lissu amekiri kupokea kiasi cha Sh.43 milioni kwa ajili ya kugharamia matibabu yake kilichochangwa na wabunge wenzake siku chache baada ya kupatwa na tatizo hilo.

Amesema kuwa kiasi cha Sh. 250 milioni alizowahi kulipwa ni mshahara na stahiki zake pekee na sio fedha za matibabu kama ilivyotafsiriwa.

“Ukweli pekee uliopo ni kwamba, Bunge halijawahi kunilipa hata senti moja ya gharama za matibabu yangu. Hata senti,” Lissu anakaririwa.

Alieleza kuwa moja kati ya vikwazo vilivyowahi kutajwa kuwa kikwazo cha malipo hayo ni pamoja na kukosa nyaraka muhimu ambazo hakuziomba, ikiwa ni pamoja na kibali cha madaktari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, kibali kutoka Wizara ya Afya pamoja na Ikulu.

Wiki hii, Spika wa Bunge, Job Ndugai alimtaka Lissu kuacha kusambaza uongo kuwa hajawahi kulipwa fedha akiwa anatibiwa, akieleza kuwa ameshapewa kiasi cha Sh. 250 milioni pamoja na Sh. 43 milioni za michango ya wabunge wenzani.

Spika Ndugai alisema kuwa hivi sasa amejipanga kujibu kile alichoeleza kuwa ni uzushi wa mbunge huyo dhidi ya Bunge, na kwamba endapo atapinga kupokea malipo hayo atakuja na vielelezo alivyoviita ‘mkeka’.

Video: Diamond awashukia wasanii wanaopeleka hongo Wasafi TV
Video: Makonda kumsweka ndani Harmonize, 'Haiwezekani avute bangi'