Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika ‘TLS na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ameendelea na msimamo wake wa kulaani tukio la kuvamiwa Ofisi za Wanasheria IMMMA Advocates huku akiungwa mkono na kituo cha haki za binadamu LHRC na kusema kuwa ni muhimu jambo hilo likapigiwa kelele kwakuwa siyo la kisiasa.

Ameyasema hayo mara baada ya kualikwa katika mkutano wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na kusema kuwa kuna mashirika mengi yasiyokuwa ya kiserikali ndani ya Tanzania ambayo yanafanya kazi za kutetea haki za binadamu lakini wengi wao katika tukio hilo wamekuwa kimya.

“Wengi katika tukio hili wamenyamaza na kuogopa, kituo cha Sheria na Haki za Binadamu wamesimama hadharani na kupaza sauti zao kwa hichi kilichotokea cha kuvamiwa Mawakili. Sasa naomba nitoe pongezi za dhati kabisa kwa kituo cha haki na binadamu kwa kuwa mtetezi wa kweli kwa Mawakili wanaoshambuliwa pamoja na kuwaunga mkono Mawakili wetu katika kipindi hiki kigumu. Maana mtetezi wa kweli utamjua wakati umeshambuliwa,”amesema Lissu

Hata hivyo, kwa upande mwingine, Lissu amesema kuwa mwaka huu 2017 wametunga sheria inayosema kila mtu mwenye kesi Mahakamani anastahili kupata msaada wa kisheria wa Mawakili ila anashangaa wanapowashambulia Mawakili hao.

Neno SHIELD Larekebishwa Ngao Ya Jamii
Umoja wa Ulaya waunda mpango wa kukabiliana na wahamiaji haramu