Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu, amesema kuwa Rais wa zamani wa Cuba  Marehemu Fidel Castro alikuwa ni mwamba mkubwa kwenye siasa za dunia, ameongeza  kuwa nchi ya Cuba imekuwa ikitoa kipaumbele katika kusaidia nchi zinazoendelea.

Lissu alisema Cuba ya Castro imepeleka madaktari na wafanyakazi  wengi kwenye nchi zinazo endelea na masikini  kuliko nchi nyingine yoyote duniani,kwaajiri ya kusaidia kupigania uhuru kwa nchi nyingi za kiafrika ambazo zilikuwa bado mikononi mwa wakoloni.

Aidha, aliongeza kuwa licha mataifa makubwa ya Magharibi na Urusi, Cuba iilkuwa nchi pekee kufanya programu ya millitary power nje ya bara lake ili kutetea uhuru wa nchi hizo.

 

 

Gerard Pique Ahofia Kupoteza Ubingwa
Ricardo Kaka Asaka Heshima Orlando City