Mbunge wa Singida Mashariki, Tindu Lissu amesema kuwa atafanyiwa upasuaji wa 19, Machi 14 mwaka huu ili kuondoa hatari ya mfupa kutounga vizuri.

Kupiti ukurasa wake wa Instagram, Lissu amesema kuwa madaktari wake bingwa wa mifupa wamependekeza afanyiwe upasuaji mwingine kwenye mfupa wa juu ya goti la kulia baada ya kubaini kuwa kasi ya mfupa huo kuunga ilikuwa hairidhishi.

Amesema kuwa yuko salama chini ya madaktari bingwa wa mifupa wanaoaminika barani Ulaya, Prof. Dkt Stefa nijs na Prof. Dkt, Willen Jan Maertsemakers. Upasuaji huo utafanyika katika Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, Gasthuisberg nchini Ubelgiji.

“Hivyo, msiwe na hofu. Mungu wetu aliyeniwezesha kuwa hai sasa, ataendelea kutenda miujiza upitia kwa madaktari bingwa hawa,” Lissu ameandika.

Mwanasiasa huyo ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) alishambuliwa kwa risasi Septemba 17, nje ya nyumba yake mjini Dodoma.

 

Black Panther yazidi kupaa, yapiga $bilioni 1
Wafugaji waua wakulima watano kwa risasi

Comments

comments