Mgombea Urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Tundu Lissu, amewashukuru na kuwakumbusha wananchi wa Babati, kujitokeza kwaajili ya kupiga kura zikiwa zimesalia siku 9 kuelekea Uchaguzi mkuu Oktoba 28, 2020.

Akihutubia umati uliojitokeza kusikiliza sera zake Oktoba 18,2020, Lissu amewashukuru wananchi hao kwa maombi, misaada pamoja na sala zao kwa kipindi chote cha miaka mitatu alichokuwa akikipitia.

“Nawashukuruni sana kwa maombi yenu, kwa misaada yenu ya kila namna, kwa sala zenu katika kipindi hiki cha miaka mitatu nilichokipitia, ndugu zangu wa Babati zimebaki siku kumi mtapiga kura katika mazingira hayahaya” amesema Lissu

Aidha Lissu, ameendelea kuwahimiza wananchi kujitokeza kupiga kura ifikapo tarehe 28 mwezi huu huku akiainisha baadhi matukio ambayo hutokea katika siku ya uchaguzi ikiwemo ya mawakala kutokuruhisiwa kuingia vituoni ambapo amesema kwa mwaka huu kwa mujibu wa kanuni za Tume ya Taifa ya Uchaguzi barua ya utambulisho wa mawakala zitapelekwa na Mkurungenzi wa uchaguzi katika vituo.

Azam FC yatua Mbeya, kuikabili Ihefu FC kesho
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 19, 2020