Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu amesema anatarajia kuwasili nchini Januari 25, 2023, ili kushiriki shughuli za siasa za chama hicho.

Lisu, ambaye alikuwa akitoa salaam za mwaka mpya akiwa nchini Ubelgiji amesema, “Panapo majaliwa, nitakanyaga udongo wa ardhi ya Tanzania kwa mara nyingine tena siku ya Jumatano ya tarehe 25 Januari, 2023, majira ya saa saba na dakika 35 mchana.”

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.

Amesema, anampongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuonesha nia ya kuleta mageuzi ya kisiasa nchini, ikiwemo kukwamua mchakato wa katiba watawajibika kumjibu kwa kuonesha, na kudhihirisha kwa vitendo, jinsi walivyojiandaa kwa safari hiyo.

“Ninarudi nyumbani kuja kushiriki katika kuandika ukurasa wa kwanza mpya wa kitabu chenye kurasa 365 cha mwaka huu wa 2023. Ninaamini kwamba, kwa umoja wetu na kwa mapenzi yetu kwa nchi yetu, tutaandika kitabu kizuri,” amefafanua Lissu ambaye alikuwa akizungumza kwa njia ya mtandao.

Mvulana (17) akamatwa kwa kuwapa ujauzito wanawake 10
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Januari 14, 2023